DCEA wapongezwa kwa kazi nzuri mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini

DAR ES SALAAM-Februari 29,2024 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga ametembelea makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Naibu waziri Mhe. Ummy amewapongeza watumishi kwa juhudi zao na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kupambana na dawa za kulevya nchini.

Sambamba na pongezi hizo, Mhe. Ummy amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuhakikisha mamlaka inaimarika kiutendaji ili kupata mafanikio zaidi.

Aidha, amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi, weledi, na kuwa wazalendo ili kutekeleza azma ya Serikali katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news