NA DIRAMAKINI
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko ameteua wajumbe nane wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Dkt.Biteko amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu Namba 9 (1) na (3) cha Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992 (The Public Corporation Act of 1992).