ARUSHA-Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imewataka wadau wake wote kupuuza taarifa iliyosambaa mitandaoni ikidai kuwa imetambulisha noti mpya ya pamoja itakayotumika katika nchi wanachama iitwayo SHEAFRA.
"Sekretarieti ya EAC inapenda kuwafahamisha wadau wetu wote kwamba safari ya nchi wanachama katika kutumia sarafu moja bado kazi inaendelea.
"Tafadhali puuzeni uvumi wowote unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuzindua noti mpya za eneo hili.
EAC ni jumuiya ya kiserikali inayoundwa na nchi saba za Afrika Mashariki ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania.