DAR ES SALAAM-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimefungua kituo cha kudhibiti madini katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kitakacho kuwa chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Madini Congo (CEEC).
Kituo hicho kinatarajiwa kuongeza ustawi wa TPA katika kuwezesha usafirishaji na biashara kati ya Tanzania na Congo, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. George Fasha amesema.
“Tukichukulia namba toka mwaka 2018/2019, tukiangalia kipi kilitoka kipi kiliingia kwa DRC, tulipitisha tani milioni 1.9, lakini kwa mwaka tulioufunga 2022/2023 wenzetu wa DRC wametumia Bandari ya Dar es Salaam kwa kupitisha mizigo yenye thamani ya tani milioni 3.4 hili ni ongezeko kubwa sana,” alisema Dkt. Fasha.