ZANZIBAR-Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amevipongeza Vikosi vya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Zimamoto na Uokozi na Chuo cha Mafunzo kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa, masoko na vituo vya wajasiriamali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Machi 9,2024 akizungumza na Maafisa na Wapiganaji alipowatembelea Vikosi vya Zimamoto na Uokozi, JKU na Chuo cha Mafunzo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amehimiza umuhimu wa nidhamu, uzalendo, uadilifu na umoja kwa Maafisa na Wapiganaji hao.