Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha aongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa

JOSEPHINE MAJURA NA ASIA SINGANO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji, Dkt. Natu El Maamry Mwamba ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) jijini Dodoma.

Aidha, kupitia kikao hicho wajumbe walipokea na kujadili hatua iliyofikiwa ya utejkelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Tasisi ya TradeMark Africa (TMA) pamoja na masuala mbalimbali ya kibiashara yenye lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) na Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo kilijumuisha Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TBS, TRA, TMX, TIC, TAFA, EPZA, TAHA, Women Chamber of Commerce.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akizungumza wakati wa kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), kilichowakutanisha Maafisa wa Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali, sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo na Sekretarieti ya TMA, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TBS, TRA, TMX, TIC, TAFA, EPZA, TAHA, Women Chamber of Commerce kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El Maamry Mwamba, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkaazi wa taasisi ya Trademark Afrika (TMA), katika Kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), kilichowakutanisha Maafisa wa Wizara na Taasisi mbali mbali za Serikali, sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo na Sekretarieti ya TMA kujadiliana masuala mbali mbali ikiwemo ikiwemo Soko la Bidhaa Tanzania kama sehemu ya kukuza uchumi wa nchi.
Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. James Msina akiteta jambo na Kamishna Msaidizi idara ya Usimamizi wa Madeni Bw. Nuru Ndile baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mhe. Dkt. Natu El Maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi Mkaazi wa taasisi ya Trademark Afrika (TMA), baada ya kumaliza Kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee) ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), inayosimamia miradi inyofadhiliwa na misaada kutoka Taasisi ya Trademark Afrika kilichofanyika jiini Dodoma.

Kikao hicho kiliwakutanisha Maafisa wa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo na Sekretarieti ya TMA, huku ikijumuisha Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TBS, TRA, TMX, TIC, TAFA, EPZA, TAHA, Women Chamber of Commerce.
Baadhi ya wajumbe waliyoshiriki kwenye kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee), ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt Natu El-maamry Mwamba wakati akiongoza kikao hicho jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe waliyoshiriki kwenye kikao cha Kamati Tendaji ya kitaifa (National Oversight Committee), ya Taasisi ya Trademark Afrika (TMA), baada ya kumaliza kikao kilichofanyika jiini Dodoma.

Aidha, Mwenyekiti wa Kikao hicho Dkt. Natu Mwamba alisisitiza taasisi hiyo kuendelea kutekeleza miradi ambayo ina manufaa mapana kwa taifa na inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news