Kinana afunguka kuhusu uchaguzi huru na haki

DAR ES SALAAM-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia Watanzania kuwa serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufanya uchaguzi huru na wa haki kuanzia wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.
Kinana ameyasema hayo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu wa chama cha ACT -Wazalendo.

"Tunakwenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye mwakani uchaguzi mkuu. Kumefanyika mabadiliko ya sheria tatu bungeni. Sheria ya vyama vya siasa, sheria ya tume ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi.

"Kuna maoni yametolewa na wadau mbalimbali katika kamati za bunge, bungeni...ukiangalia sheria ile baada ya maoni na ushauri kuna mabadiliko makubwa sana.
"Nataka niwahakikishie kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ina dhamira ya dhati katika mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao kwenye serikali kuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki," amesema Kinana.

Amesema,mbali na kupitisha sheria nzuri ya kuhakikisha kunakuwapo uchaguzi huru na wa haki, pia dhamira ya Rais Dkt.Samia kufanikisha hilo inajipambanua katika utekelezaji wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news