LAAC yatoa agizo mkoani Shinyanga

SHINYANGA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeagiza ifikapo Septemba,2024 ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Shinyanga uwe umekamilika.
Agizo hilo limetolewa na Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Staslaus Mabula wakati akikagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mhe. Mabula ameitaja miundombinu inayotakiwa kukamilishwa kuwa ni mabweni, bwalo, uboreshaji wa nyumba za walimu na ukamilishaji wa miundombinu ya kuvunia maji ya mvua.
Aidha, Kamati imeridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.3

Akizungumzia ukaguzi uliofanywa katika mradi wa ujenzi wa soko kuu, Mhe. Mabula amesema Kamati imeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwa na andiko la mradi linaloanisha gharama zitakazotumika kukamilisha mradi wote pamoja na makusanyo ya mwezi na mwaka.
Kamati ya LAAC imefanya ziara katika mikoa ya Kagera, Geita, Simiyu, Mara na Sinyanga kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo 23 inayotekelezwa katika halmashauri 12.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news