MOROGORO-Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro,Shaka Hamdu Shaka amelazimika kutembea zaidi ya kilomita tano ndani ya maji.
Ni wakati wakiwa katika harakati za kusaidia kuokoa wananchi waliopata mafuriko kufuatia kujaa mto Miombo baada kupokea maji mengi kutoka milimani.

Hata hivyo, wakati wakitoka eneo hilo wakajikuta wamezungukwa na maji na kulazimika kuanza kutembea kujinusuru sambamba na kuwasaidia wananchi wengine ambao bado walikuwa katika makazi yao.
