NA GODFREY NNKO
ZAIDI ya wanawake 40 wamewasilisha majina yao kwa Senior Elisaria Palllango ili aweze kuyapeleka kwa Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha wa Kanisa la Fresh Spring Fellowship (Ngome ya Yesu Kristo) lililopo Kimara Temboni aweze kuwaokoa katika biashara ya ukahaba jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainika leo Machi 25,2024 kupitia Kipindi cha Satelite kinachorushwa na Redio Classic FM iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Katika kipindi hicho, mmoja wa makahaba hao aliyejitambulisha kwa jina la Merryciana Paul amesema, kazi hiyo ya kuuza mwili wake ameifanya kwa miaka mitatu huku akiambulia maumivu badala ya faida.
Hayo yanajiri ikiwa Kuhani Musa amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na kipawa alichopewa na Mungu ambapo amekuwa akiwatoa watu wengi katika vyama mbalimbali ikiwemo vya kichawi.
Merricyiana amesema, kitu ambacho kinamuumiza zaidi ni kwamba, kilichomsukuma kujiiingiza katika ukahaba na uduni wa maisha ukizingatia kwamba hakuweza kusoma.
Amesema, kati ya matukio ambayo yanamuumiza moyo wake, hivyo kuona Yesu ni kimbilio la maisha yake ni baada ya siku moja kuchukuliwa na mwanaume kwenda kumpa huduma, lakini alipofika chumbani alikutana na wanaume watatu.
Anasema, alipouliza kulikoni, aliabiwa tulia ndipo wanaume hao waliamua kumchania nguo na kuanza kumshughulikia kwa zamu, hivyo kujikuta katika hali mbaya na kupelekwa hospitali.
"Sikuwa na namna. Nilipotoka hospitali nilirejea tena kujiuza."
Akizungumzia kilichomsukuma kuandika jina lake na kutaka lipelekwe kwa Kuhani Mussa kwa ajili ya kuombewa na kuondolewa katika ukahaba, Merricyiana amesema kuwa,ameona ni vema kuanza upya na Mungu na kumaliza na Mungu.
Amesema, kila anapoota amekuwa akiota ndoto nyingi ambazo zimekuwa zikimtesa maisha yake ikiwemo kuzaa watoto wazuri na kushiriki tendo la ndoa na wanaume kila saa.
Akizungumzia kuhusu ndoto ambazo Merryciana anaoteshwa za watoto, Senior Elisaria Palllango amesema,ndoto za kuzalishwa watoto wa kijini zinaashiria mfumo kamili wa kijini ambao amewekewa.
"Nikupe pole sana Merryciana, lakini pia nikupe hongera kwamba umeamua sasa hautanyamaza, utapiga kelele na kupaza sauti kwamba sasa unapambana na kupinga hayo mambo."
Hata hivyo, Senior Elisaria Palllango amemshauri Merryciana na wenzake kuendelea kutulia wakati taarifa hizo zinatarajiwa kumfikia mtumishi wa Mungu,Kuhani Mussa.
Lengo likiwa ni kuona namna ambavyo itapangwa ibada maalumu ili waweze kusaidiwa kujitoa katika biashara ya kuuza miili yao.
Ameongeza kuwa, "Mwanamke yeyote ambaye anajiuza ukifuatilia aina ya ndoto ambazo wanaziota utakuta kwamba kuna kazi maalumu ambayo anafanyishwa.
"Kwa mfano, yeye (Merryciana) pamoja na kujiuza usiku mzima akienda tu kujilaza huyo manaume anakuja pia, yaani anaangaika kujiuza, lakini akilala tu kuna wanaume wengine ambao wanakuja.
"Na kama alivyosema (Merryciana) kwamba anaota amezaa watoto wazuri, lakini pia anawanyonyesha wale ni majini.
"Na wanaume ambao anazaa nao ni wale ambao wanakuja sasa kwenye usingizi, kwa hiyo majini kamili yanakuja kwa namna ya mwili na wanazaa naye.
"Sasa, majini yanapotembea na yeye maana yake yanachochea ile kazi ambayo ni ya giza, kwa hiyo huyu kitu cha kwanza kabisa hata kama ukimpa hela.
"Kama hajafanyiwa ukombozi zitaisha maana yake monitoring yake ipo kwenye ulimwengu wa kipepo, sasa hao ndiyo watu ambao wanahitaji msaada maana yake wanatumika duniani, anatumika kuzimu na hamna faida yoyote ambayo anaweza kuiona."
Tags
Fresh Spring Fellowship Kimara Temboni
Habari
Kuhani na Mwalimu Richard Mussa Mwacha
Makuhani Tanzania