ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi amezindua programu ya kugawa taulo za kike (Tumaini Kits) katika viwanja vya Jadida Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa, Mkuu wa UNICEF Zanzibar Laxmi Bhawani na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib.