ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameitaka jamii kuchukua jitihada za makusudi kuhakikisha wanaepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Miongoni mwa magonjwa hayo ni kisukari, moyo, shinikizo la damu na mengineyo ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa familia na Serikali.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo Machi 8,2024 wakati akifunga kambi ya siku tano ya Matibabu ya "Afya Bora, Maisha Bora" iliyohudumia zaidi ya wananchi 5000 chini ya Taasisi ya ZMBF.
Sambamba na kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Viwanja vya Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aidha,Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wananchi umuhimu wa kuzingatia lishe bora hususani wanawake walio katika umri wa kubeba ujauzito ili kupunguza hatari ya kupata safura, utapiamlo na udumavu kwa watoto.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
Zanzibar News