Meli bandarini zaongezeka kutoka 4,318 hadi 4,762 nchini

NA GODFREY NNKO

SERIKALI imesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan meli bandarini zimeongezeka kutoka 4,318 Machi 2021 hadi kufikia meli 4,762 Februari 2024 sawa na ongezeko la asilimia 10.28.

Aidha,kiwango hiki cha ukuaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 11.79 kwa mwaka.Hayo yamesemwa leo Machi 24, 2024 jijini Dar es Salaam na Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarani.

Amesema, shehena iliyohudumiwa iliongezeka kutoka tani milioni 17.287 Machi 2021 hadi kufikia tani milioni 26.544 Februari 2024, sawa na ongezeko la asilimia 37.9.

"Kiwango hiki cha ukuaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 15.4 kwa mwaka."

Vile vile,Matinyi amesema shehena za makasha na shehena za magari ziliongezeka.

"Shehena ya nchi jirani iliongezeka kutoka tani 6,166,052 Machi 2021 hadi kufikia tani 9,452,535 Februari 2024, sawa na ongezeko la asilimia 53.3.

"Kiwango hiki cha ukuaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 26.5 kwa mwaka."

Pia, amesema katika kipindi cha Awamu ya Sita, Serikali imeweza kukamilisha ujenzi wa gati maalumu la kuhudumia meli za magari (Gati Na. 0), uboreshaji wa gati Na. 1 – 4 kwa ajili ya kuhudumia shehena mchanganyiko, gati Na 5 – 7 kwa ajili ya kuhudumia shehena ya makasha,

“Kuongeza kina cha gati 1-7 kutoka mita 11 hadi kufikia mita 14.5, na kukamilika kwa ujenzi wa yadi ya kuhudumia makasha, kuchimba na kupanua lango la kuingilia meli na sehemu ya kugeuzia meli,” amesema Matinyi.

Amesema, mbali ya Serikali kuongeza vifaa vya kisasa, lakini pia kuna upanuzi wa bandari za Tanga, Mtwara, na zile za maziwa ili kukidhi mahitaji ya soko katika nchi jirani ambayo yanaongezeka siku hadi siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news