Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) waleta matokeo chanya Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imefanikiwa sana kuongeza ukaribu na wananchi kwa kusikiliza changamoto na kuzitatua kwa haraka kupitia Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR).
Amesema,Mfumo wa SNR ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi pia ni kigezo cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji wa wananchi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi 16,2024 Ikulu jijini Zanzibar katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 3 ya Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR).
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kitengo cha SNR kina wajibu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia njia mbalimbali kwa wananchi ili waweze kutumia vema Mfumo huu kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 3 tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa SNR jumla la malalamiko 13,517 yamepokelewa kati ya hayo 11,116 yamepatiwa ufumbuzi na 2,351 yanaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama na Vyama vya Siasa wamehudhuria hafla hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news