IRINGA-Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Utamaduni, Sanaa,Hamasa na Michezo ya Baraza Kuu la Wazazi Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Mgongolwa ametoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Sambamba na familia wakiwemo Watanzania kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kilichotokea Februari 29,2024 jijini Dar es Salaam.
"Nitoe pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia, kwa familia na Watanzania wote kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alihudumu kati ya mwaka 1985 hadi 1995, Mheshiwa Ally Hassan Mwinyi ambaye amefariki dunia Alhamisi ya tarehe 29 Febuari 2024.
"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya baba na babu yetu huyu mahali pema. Hakika, Watanzania tutamkumbuka daima,"amefafanua Mgongolwa.
Mgongolwa amefafanua kuwa, hayati Rais mstaafu Mwinyi atakumbukwa kwa mengi ikiwemo kufungua uchumi na siasa za Tanzania na Zanzibar.
Vile vile, kupitia Azimio la Zanzibar aliruhusu uchumi wa soko.
"Na diye aliyeunda Tume ya Nyalali ili kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa na kuruhusu uhuru wa habari na vyombo binafsi vya habari nchini."
Amesema, wakati wa uhai wake katika utumishi wa umma Mzee Mwinyi alipitia changamoto mbalimbali ambazo aliweza kuzishinda ikiwemo kuwajibika na kuwajibisha kwa maslahi ya Taifa.