LUANDA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 hadi 5 Machi, 2024.
Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha tarehe 6 Machi, 2024 ambapo kwa pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2024 jijini Luanda, Angola.

Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.