Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani awasili nchini kwa ziara ya kikazi

KILIMANJARO-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul amewasili nchini tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makori alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Keul amelakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makori, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta na viongozi wengine wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.

Akiwa nchini Mhe. Keul atatembelea Hospitali ya KCMC, kuzuru kaburi la Mangi Meli na kutembelea Parish ya kidia ambako atahudhuria sherehe za kukumbuka maisha ya kazi za mwandishi wa Ujerumani mchungaji Bruno Gutmann aliyeishi eneo hilo kwa miaka 28 na kuzindua kitabu cha maisha ya kiutamaduni ya wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya America na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Naomi Zegezege alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makori (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta (wa pili kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.

Mhe. Keul pia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Mazungumzo yakiendelea katika chumba cha kupumzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Ziara ya Mhe. Keul pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pia inalenga kuendelea kuimarisha Uhusiano na ushirikiano Kati ya Tanzania na Ujerumani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news