NHC yaendelea kugusa maisha ya wengi,yakabidhi futari kwa wananchi

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kugusa maisha ya makundi mbalimbali ya kijamii nchini ambapo leo Machi 21, 2024 wamekabidhi futari kwa wananchi katika Msikiti wa Masjid Al Jumuiya Al Madina uliopo Mbezi Msakuzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusiana na msaada huo, Afisa Uhusiano kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi.Yamlihery Ndullah amesema, "Shirika la Nyumba la Taifa tuna sera yetu ya kurejesha kidogo tunachokipata kwa jamii. 

"Kwa maana ya Cooperate Social Responsibility (CSR) ambapo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tumeona tuje tutoe kidogo tunachokipata kwa ndugu zetu ambao wanafunga kwa mwezi huu.

"Kwa hiyo, Shirika la Nyumba la Taifa leo tupo hapa katika Msikiti wa Masjid Al Jumuiya Al Madina uliopo Mbezi Msakuzi, tumeleta futari yetu ndogo ambayo imeambatana na daku ambayo itatumika katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
"Tumeleta unga wa ngano, tumeleta maharage, tumeleta mchele, tumeleta tambi, tumeleta sukari pamoja na kunde, ambavyo hivi vitatumika kwenye futari na pia kwenye daku,"amesema Bi.Ndullah.

Mwakilishi

Akipokea sadaka hiyo katika Masjid Al Jumuiya Al Madina, Jumaa Salum Mhando amesema kuwa, "Sadaka hii ni kwa ajili ya watoto, lakini sasa hivi hawapo, lengo ni kuwawezesha kuwakwamua katika hali waliyonayo katika maisha kwa sababu wanaishi katika mazingira magumu.

""Nitoe shukurani kubwa, za dhati kwa ndugu zangu hawa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kutujalia hii neema na hususani wameileta katika wakati maalum kwa sababu tupo katika wakati maalum, tupo katika siku za kuchuma heri nyingi.
"Na, ninaamini kabisa waliofanya hili, watapata zaidi ya haya kwa sababu aliyetoa kimoja atalipwa kumi, sasa hapa NHC wametoa zaidi ya haya ambayo tunayaona, basi watalipwa zaidi.

"Kwa sababu, huu ni mwezi wa baraka, na kikubwa zaidi ni kuwaombea NHC kwa Mwenyenzi Mungu azidi kuwafanyia wepesi katika kazi zao na awaruzuku mbadala.

"Kwa sababu anayetoa huwa hapotezi bali anayetoa kwa nia kusaidia, Allah anamuongezea. Kwa hiyo, katika hili ninawaombeni ndugu zangu mpeleke salamu kwa ndugu zangu wengine ambao wanaguswa na hili, wawasaidie hawa ndugu zetu ambao wana mazingira magumu.

"Wawasaidie hususani katika huu mwezi wa Ramadhani kwa sababu kuna fadhila nyingi sana zinapatikana, mwenye kutoa sadaka basi huyu, Allah anamuongezea.

"Kwa hiyo, ninawaombeni vile vile muendelee kutusaidia kwa sababu bado tuna mahitaji mengi, hapa tulipo tuna mahitaji mengi, kituo hiki bado hakijaisha, madrasa ile haijaisha na kuna mambo mengi ambayo yanahitajika, kwa hiyo ninachowaombeni ndugu zangu mtufikishie taarifa hizi kwa wengine kwamba tunahitaji misaada yenu.

"Hususani katika huu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kutukwamua katika hii hali tuliyo nayo, kwa sababu licha ya sadaka hii kubwa ambayo tumepata hapa, bado kuna mahitaji mengine ambayo tutahitaji,wadau wengine waweze kutusaidia.

"Kwa sababu ninajua wapo watu wengi na nina mahitaji mengi, na hii ni desturi yetu sisi hapa huwa kila mwezi wa Ramadhani tunapokea sadaka mbalimbali na vile vile tunawapa wale wenye mahitaji, na wengine wanafuturu hapa hapa na wale waliopo majumbani vile vile tunawapelekea."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news