Chuo Kikuu Huria cha Nigeria (NOUN) kimemualika Profesa Elifas Bisanda wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kutoa mada kuhusu: IWAPO ELIMU YA ULAYA MAGHARIBI BADO NI MUHIMU KWA NCHI ZA BARA LA AFRIKA. Mada hiyo ataitoa wakati wa wiki ya sherehe ya mahafali ya chuo hicho yatakayoanza Aprili 13, mwaka huu mjini Abuja.