ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametaja baadhi ya mambo aliyojifunza kutoka kwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hayati Ali Hassan Mwinyi wakati wa uhai wake.
"Hayati mzee Mwinyi alikuwa na subira kubwa wakati alipokuwa kiongozi hususani kipindi cha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.
Pia,watu walimsema vibaya kwa mambo ya kutunga katika vyombo vya habari,lakini hakuwahi kumjibu yeyote kwa mabaya waliyomsema."
Alhaj Dkt.Mwinyi ameongeza na kusema yeye amejifunza kusubiri kwa fundisho alilolipata kwa mzee wake kwa kumpa mafunzo mema.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema wakati marehemu baba yake alipokuwa akitibiwa Uingereza aliwataka madaktari na familia arudishwe nyumbani na baadae apelekwe Zanzibar, maneno hayo aliyarudiarudia hata baada ya kufika Dar es Salaam.
RaisDk.t. Mwinyi ameyasema hayo katika dua ya hitma iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hayati Ali Hassan Mwinyi ambayo imefanyika leo Machi 5,2024, Msikiti wa Zinjibar Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.