ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Machi 5,2024 amepokea salamu za pole nyumbani kwake Ikulu Migombani jijini Zanzibar kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali John Jacob Mkunda.
Ni kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Ali Hassani Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29, 2024 jijini Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2, 2024, Mangapwani huko Mkoa wa Kaskazini, Unguja.