ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema, misikiti inatakiwa kutumika kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo Machi 8,2025 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na kufungua Msikiti wa Masjid Itiswaam Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia Misikiti kufanya ibada kwa wingi hususani kuelekea kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema kuna wajibu wa kuwafundisha watoto elimu ya dini mapema.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa shukrani kwa wafadhili waliofanikisha ujenzi wa msikiti huo.