NA FRESHA KINASA
MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly amekabidhi vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika Shule ya Msingi Butiama 'A' iliyopo Wilaya ya Butiama.

Rhobi amekabidhi vifaa hivyo Machi 6, 2024 akiwa ameongozana na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Butiama.

"Nilipokea maombi uongozi wa shule wakiniomba vifaa hivi kusudi viwasaidie wanafunzi wenye mahitaji Maalumu shileni hapa. Nami kwa kutambua umuhimu na thamani ya elimu nimeleta vifaa hivi naamini kabisa vitakuwa na msaada mkubwa kwa wanafunzi hawa ambao ni tegemeo kwa Taifa letu."amesema Rhobi.

Pendo Wambura ni Mwalimu wa Kitengo cha Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Butiama 'A' amemshukuru Rhobi Samwelly kwa kutoa vifaa hivyo ambapo amesema, vitawezesha wanafunzi hao kusoma vizuri tofauti na awali.

Naye Jane Mbura ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Butiama amesema kuwa Jumuiya hiyo imeamua kutumia maadhimisho ya siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka kutoa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na mahitaji kwa wagonjwa Katika kituo cha afya Kiagata..jpg)
.jpg)
Amesema,jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau mbalimbali wanaopambana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia na kuimarisha haki za binadamu ili kujenga usawa katika jamii.