Rhobi Samwely amzawadia mtoto mwenye mahitaji maalumu kiti mwendo na godoro

NA FRESHA KINASA

MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia lenye makao makuu yake Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, Rhobi Samwely amekabidhi msaada wa kiti mwendo (Wheelchair) na godoro la kulalia kwa mtoto Sabato Matiku mwenye ulemavu wa miguu na mikono anayeishi na wazazi wake Mugumu Mjini.
Rhobi amekabidhi msaada huo Machi 7, 2024 nyumbani kwa wazazi wake akiwa na viongozi na wanawake wa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimisha kila mwaka Machi 8.

Pia, ametoa wito kwa wadau kuendelea kuwasaidia watoto na watu wenye ulemavu na mahitaji mbalimbali katika jamii.

"Mtoto huyu ambaye hawezi kutembea wala kukaa pasipo usaidizi, hivyo baiskeli hii itakuwa na msaada mkubwa kwake. Nitoe woto kwa wadau na watu mbalimbali tuendelee kuwasaidia watoto na watu wenye ulemavu wa viungo mbalimbali,"amesema Rhobi na kuongeza kuwa.
"Neno la Mungu linatufundisha kupendana, kujaliana na kuthaminiani tunapofanya kwa vitendo inapendeza sana. Wapo wengi wenye uhitaji maeeno mbalimbali ni wajibu wetu kuwapa sapoti. Wao ni sehemu ya jamii yetu tusiwatenge wala kuwabagua,"amesema Rhobi.

Pia, Rhobi ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowanyima fursa ya elimu watoto wenye ulemavu kwani wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii iwapo watawekewa mazingira wezeshi na rafiki kusudi watimize ndoto zao.
Mzazi wa kijana huyo Ghati Ryoba Matiku, amemshukuru Rhobi Samwelly kwa msaada huo na kusema hakuwa na uwezo wa kununua baiskeli hiyo kutokana na uchumi na kupelekea mwanaye kuishi kwa tabu kubwa. Lakini kwa Sasa anafuraha kuona mwanaye amepata msaada huo.

Angelina Marko ni Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti amempongeza Rhobi Samwelly kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia wahitaji. Huku akisema kuwa serikali Wilayani humo itahakikisha Kijana Sabato anasoma kusudi atimize ndoto zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news