Serikali yaagiza mafunzo Mfumo wa NeST

DODOMA-Makatibu Tawala wa mikoa nchini wametakiwa kuhakikisha wakuu wa shule za msingi na sekondari na waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya wanapewa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi (NeST) kabla ya kuanza kutumika.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa itaongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi hasa ikizingatia kuwa Serikali inakusudia kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde wakati wa kufungua mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa umma (NeST) yanayofanyika katika Ukumbi wa shule ya msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma.

Alisema,Serikali imekuwa ikipeleka fedha nyingi za kutekeleza miradi katika ngazi ya mzingi hivyo Ma-RAS, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara ya halmashauri kuhakikisha wanafundisha kwa ukamilifu wale wote wanaotekeleza shughuli za manunuzi katika ngazi ya msingi wakiwemo wakuu wa shule.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news