MBABANE-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Eswatini zimekubaliana kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 30,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Hayo yalielezwa Machi 28,2024 wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msumbiji, Eswatini na Madagascar na Mhe. Pholile Shakantu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Eswatini uliofanyika jijini Mbabane.
Ili kufanikisha azma hiyo, viongozi hao wamekubaliana kuanzisha mchakato wa kusainiwa Mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) inayohusisha sekta mbalimbali baina ya nchi hizo mbili.