ACCRA-Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Ofisi ya Hakimiliki ya nchini Ghana ikiongozwa na William Bonsu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na baadhi ya wataalamu wa Hakimiliki wa nchi hiyo.

Amefanikiwa kujifunza namna nchi hiyo inavyokusanya mirabaha kwa kutumia Kampuni za Kukusanya na Kugawa Mirabaha (COLLECTIVE MANAGEMENT ORGANISATION -CMO'S) na kuzisimamia ambapo pia Tanzania inafanya jambo kama hilo kwa Wasanii na Wabunifu kupitia Kampuni ya TAMRISO inayokusanya mirabaha ya wanamuziki.