KISUMU-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya zimekubaliana na kutia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kuruhusu raia kutoka nchi hizo kufanya biashara baina yao kwa urahisi na kwa manufaa ya pande zote mbili. Makubaliano hayo yametiwa saini na Wakili Stephen Byabato Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na mwenzake Mhe. Rebbecca Miano, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda kutoka nchini Kenya. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024.
Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya watalaam kisha ngazi ya Makatibu Wakuu ambapo zaidi ya vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru zaidi ya 14 vilijadiliwa na kuwekewa mpango wa kuendelea kuviondoa vyote.