TANZIA:Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TARI,Dkt.Geoffrey Mkamillo afariki

Dkt.Geoffrey Mkamilo ambaye alikuwa na Shahada ya Uzamivu katika Ikolojia ya Uzalishaji na Uhifadhi wa Rasilimali.Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Alifanya kazi kama Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Utafiti wa Muhogo ambapo jukumu lake kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kuwa utafiti wa zao la muhogo unafanyika kwa mshikamano na ufanisi nchini, hivyo kuwaongoza watunga sera katika Wizara ya Kilimo kufanya maamuzi sahihi ya kitaifa kuhusu zao la muhogo.

Vile vile alikuwa na uzoefu mkubwa katika utafiti na alishiriki katika kozi nyingi zilizoundwa maalum zikihusisha kilimo, ufugaji na uchambuzi wa takwimu na nyinginezo.

Februari mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt.Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) akichukua nafasi ya Dkt. Geoffrey Mkamillo ambaye alimaliza muda wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news