NA MUNIR SHEMWETA
KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema, wizara yake itahakikisha inatoa Hatimiliki za Ardhi katika maeneo yote Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unatekelezwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Mhe.Japhet Hasunga wakati wa ziara ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.
Mhandisi Sanga amesema hayo leo tarehe 27 Machi 2024 wilayani Nzega wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Serikali (PAC) ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika Utekelezaji mradi wa LTIP kwenye halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora.
Kauli hiyo ya Mhandisi Sanga inafuatia baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutaka utekelezaji mradi wa LTIP unaoendelea maeneo mbalimbali nchini kwenda sambamba na utoaji hati milki za ardhi.
‘’Wananchi wa Nzega tuwahakikishie sisi kama wizara tutahakikisha muda tuliokusudia kukamilisha mradi basi hati mnapata. Wote mtazipata hati na utoaji wa hati ni hatua ya mwisho,’’ alisema Mhandisi Sanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kukagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, kazi kubwa katika utekelezaji mradi huo wa LTIP ni kutambua, kupanga na kupima na hatua hizo zikishakamilika hati zote zinakuwa kwenye mtandao.
Akielezea zaidi kuhusu utekelezaji wa mradi wa LTIP katika halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora, Mhandisi Sanga amesema kazi hiyo kwa sasa imetelekezwa kwa asilimia 55.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani) wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.
"Kwa kuzingatia ukubwa wa kazi iliyofanyika ikilinganishwa na muda uliobaki ni matarajio yetu kuwa malengo ya mradi yatafikiwa kama ilivyopangwa kwa kuwa sehemu kubwa ya kazi ambazo zinahitaji utaalamu na muda mwingi zimeshakamilika," amesema Mhandisi Sanga
Ameongeza kuwa, hadi sasa vipande vya ardhi 18,655 vimetambuliwa, vipande 8,814 vimepangwa na viwanja 3,960 vimepimwa huku Alama za Msingi za Upimaji 14 zikiwa zimesimikwa ardhini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe, Japhet Hasunga akizungumza wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.
Mradi wa LTIP katika Halmashauri ya Mji wa Nzega imepewa lengo la kurasimisha vipande vya ardhi 20,000 ifikapo Juni 30, 2024 na kuongeza alama za msingi za upimaji 14.
Urasimishaji huo unatekelezwa katika mitaa 14 iliyopo kata 5 ambazo ni Nzega Mashariki, Nzega Magharibi, Nzega ndogo, Kitangiri pamoja na mtaa wa Uchama.
Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Jumanne Mtemvu na Geofrey Mwambe wakiangalia orodha ya wananchi waliofanyiwa utambuzi katika utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika halmashauri ya Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.
Kwa sasa utekelezaji wake unaendelea kwa zoezi la uhakiki wa taarifa za wananchi katika mtaa wa Nyasa, Msoma na Kitongo na upandaji wa mawe unaendelea katika mtaa wa uwanja wa ndege.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe, Japhet Hasunga akizungumza wakati Kamati yake ilipokagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Katika Mji wa Nzega mkoa wa Tabora tarehe 27 Machi 2024.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unatekelezwa kwa mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milionin150 kutoka Benki ya Dunia kwa kupindi cha miaka 5 katika halmashauri 58 nchini. Mradi huo unalenga kuboresha utawala na usimamizi wa ardhi nchini pamoja na kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa wananchi.