DAR ES SALAAM- Ni wazi tatizo la matumizi ya dawa za kulevya limeendelea kutamalaki katika maeneo mbalimbali nchini.
Licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali na taasisi nyingine zisizo za kiserikali kupambana na tatizo hili, bado matumizi ya biashara ya dawa za kulevya yameendelea kuwepo na kushika kasi huku wahanga wakubwa wakiwa ni vijana.
Hii ndio sababu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) imeamua kuwekeza katika kutoa elimu ya dawa za kulevya kwa wanafunzi nchini.
DCEA imekuwa ikizitembelea shule mbalimbali kufikisha elimu sahihi kuhusu tatizo la dawa za kulevya nchini, lakini ili kuweza kuwafikia watoto wengi ni jukumu la kila mzazi kumpa mtoto wake elimu hiyo ili aweze kutimiza malengo yake ya kusoma;
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)