Uzalishaji wa malisho Shamba la Vikunge waivutia Kamati ya Bunge

PWANI-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya viwanda ,Biashara,Kilimo na Mifugo imeridhishwa na kazi ya uzalishaji wa mbegu za malisho ya mifugo katika shamba la serikali lililopo katika kijiji cha vikunge wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza baada ya kukagua shamba hilo Machi 19, 2024, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deogratus Mwanyika amesema kamati yake imeridhishwa na ubora wa mbegu zinazozalishwa katika shamba hilo na kuiomba wizara ya mifugo ianze kusambaza mbegu hizo kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali ili wakaanzishe mashamba ya malisho ambayo watayatumia kulishia mifugo yao wakati wa kiangazi.
Awali akiikaribisha kamati hiyo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameihakikishia kamati hiyo kwamba kwa sasa suala la uanzishwaji wa mashamba ya malisho nchini ndio kipaumbele na kuwaomba wajumbe wa kamati hiyo kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news