DAR ES SALAAM-Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza adhabu kwa wachezaji na timu mbalimbali za Ligi Kuu.
Kupitia adhabu hiyo, wachezaji wa Simba SC, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wamepigwa faini ya shilingi milioni 1 kila mmoja kutokana na kufanya vitendo vilivyoashiria imani za kishirikina.