Wajengewa uelewa kuhusu Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

SHINYANGA-Wapelelezi na waendesha mashtaka wa Serikali Mkoa wa Shinyanga wamepewa mafunzo kuhusu Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Ni juu ya kuzingatia weledi katika ukamataji, uhifadhi wa vielelezo, uchukuaji wa sampuli, uteketezaji pamoja na uwasilishaji wa vielelezo hivyo mahakamani ili kuhakikisha mashauri ya dawa za kulevya yanashughulikiwa kwa ufanisi na kufikia mafanikio.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Shinyanga Mjini leo tarehe 6 Machi, 2024, Kamishna wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bi. Veronica Matikila amesema, mafunzo haya ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Dawa za Kulevya
Kamishna huyo amesema, Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa maelekezo hayo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Kamishna Jenerali na Mkurugenzi wa Upelelzi wa Makosa ya Jinai kuhakikisha watendaji walioko chini ya ofisi hizo wanapewa mafunzo haya ili kuboresha utendaji wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news