Watumishi wanawake katika Tume ya Tehama, nchini wameungana na wenzao kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo kwa Mkoa wa Dar es Salaam maadhimisho yake yamefanyika Uwanja wa Mji Mwema, wilayani Kigamboni.
Siku hii ambayo imeadhimishwa leo Machi 8 inaongozwa na kauli mbiu ya "Wekeza kwa Wanawake, Ongeza kasi ya Maendeleo".
Siku ya Wanawake Duniani ilitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo 1977 baada ya kuibuka kwa mara ya kwanza kutoka katika shughuli za harakati za wafanyakazi mwanzoni mwa karne ya 20 huko Amerika Kaskazini na Ulaya.
Mwaka huo, Umoja wa Mataifa ulipitisha Azimio Na. 32/142, kutangaza Siku ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa kuadhimishwa kila siku ya mwaka.