Waongezewa maarifa kuhusu Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini

DODOMA-Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa lengo la kutoa maelekezo katika hatua za kufuata kwenye ufuatiliaji wa afua za maendeleo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mawasilisho wakati wa kikao hicho.

Zikiwemo hatua za kitaalamu za maandalizi ya viashiria vya utendaji wa taasisi, kuanisha utaratibu wa kusimamia takwimu zitokanazo na ufuatiliaji wa shughuli za taasisi.

Sambamba na kutoa mwongozo wa maandalizi ya taarifa za ufuatiliaji, tathmini, utekelezaji na utendaji wa Serikali.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Bw. Anderson Mutatembwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho.

Akizungumza wakati wa akifungua kikao kazi cha kujenga uelewa wa Majukumu na Upimaji wa Utendaji wa Serikali ngazi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dodoma Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Anderson Mutatembwa amesema,mwongozo huu umewasilishwa katika ngazi ya Makatibu Wakuu, 

Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi na Wasaidizi wa U&T ngazi ya wizara, hivyo ni hatua muhimu katika kupata uelewa wa pamoja juu ya mwongozo husika na kutoa maoni kabla ya kusainiwa.
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Charlton Charles Meena akitoa wasilisho wakati wa kikao hicho.

"Nisisitize kuwa, mwongozo huu umekuja wakati muafaka ambapo shughuli za U&T ndani ya Idara na Vitengo vyenu zinatakiwa kufanyika kwa ubora na viwango vinavyotakiwa,"amesema Mutatembwa.

Aidha,Mutatembwa ameongeza kuwa Mwongozo unaainisha muundo wa usimamizi na majukumu ya kila taasisi kwa ngazi za Kitaifa, Kisekta na Wizara, 

Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo majukumu hayo yanaainisha kazi zinazotakiwa kutekelezwa.

Lengo ni kukamilisha upimaji wa utendaji wa kila taasisi na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za utekelezaji na utendaji wa kila siku au pindi zinapohitajika.

"Nisisitize tena, matumizi ya mwongozo huu yatawezesha Serikali kufuatilia, kutathmini na kupima utendaji wa taasisi zote katika ngazi za kitaifa na kisekta na kujenga msingi wa uwajibikaji wa taasisi husika kwenye mchango wa maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi," ameongeza Mutatembwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, Bi. Sakina Mwinyimkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), Bw. Anderson Mutatembwa (hayupo pichani) ili kufungua kikao kazi hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, Bi. Sakina Mwinyimkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu amesema, ni vizuri kuwa na mwongozo huu ili kuweza kuwa na utendaji ulimzuri kwenye kazi kwa manufaa ya Serikali.

"Naomba uwepo wenu kikamilifu katika kulitimiza kususdi la kuwepo kwetu hapa leo, maana ukiangalia kwa mwaka wa fedha uliopita na huu shauku kubwa imekuwa kwenye namna ya utendaji wa Serikali kwenye kuratibu na kusimamia utendaji wa Serikali.

"Na ninyi wenyewe mmekuwa mashahidi,tunaporudi kule kwenye utekelezaji wa kazi zetu unaona namna ambavyo tunavyofanya kazi.

"Kwa hiyo matokeo yake tunanyang'anyana rasilimali, lakini tutakapokuwa na uratibu mzuri na utekelezaji mzuri wa sera na programu hizo changamoto tutazitatua,"amesema Bi. Sakina.
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Wilson Mahera akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho.

Akifunga kikao kazi hicho Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Wilson Mahera amewasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii.

Ni ili kumsaidi Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya tamthimini zenye uhalisia wa maeneo wanayofanyia kazi kwa lengo na kuinua Mapato ya maeneo yao na Nchi kwa ujumla.

"Unakuta kule kwenye halmashari kwa sababu tumesema ni upimaji wa Serikali na vyeo mlivyopewa ni vikubwa sana na si kwamba unasimamia tu utendaji kazi wa halmashauri unakuta maafisa kilimo hawajulikani wanawajibika kwa nani.

"Unakuta wananchi wanapata shida,kwa hiyo maana yangu ni kwamba ninyi mna majukumu makubwa ya kwenda kusaidia si masuala ya tu ya bajeti,bali na kutatua matatizo ya wananchi na mhakikishe mnaelewa hiyo miongozo yote kwa ufasaha zaidi,"amesisitiza Mahela.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news