Watumishi wanawake GST waadhimisha siku yao duniani leo

DODOMA-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa Wanawake kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi nyingi kwa umakini na kwa uaminifu mkubwa.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Machi 8, 2024 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali II iliyopo Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

"Mwanamke ni Mama pia ni Kiongozi na ni mshauri mzuri katika jamii hivyo ni wasihi wanawake wenzangu tuendelea kuchapa kazi bila woga na tusichague kazi pia tusijihisi kwamba hatuwezi kufanya kazi fulani," amesema Dkt. Gwajima.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa GST, Neema Muhagama, amewataka wanawake wa Taasisi hiyo kuendelea kujitokeza kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuongeza mchango wa wanawake kwenye maendeleo ya Taifa.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yanafanyika jijini Dodoma ambayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo *"Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news