NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amenteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Mpogole Kusiluka.
Uteuzi huo unakuja kutokana na mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameyafanya.
Kindamba anachukua nafasi ya Gillard Wilson Ngewe ambaye atapangiwa kazi nyingine.