Waziri Mavunde atumia saa sita kutatua mgogoro wa wachimbaji madini Malera wilayani Tarime

MARA-Waziri wa Madini,Mhe. Anthony Mavunde leo Machi 25, 2024 amefika katika eneo la Malera lililopo Wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa Leseni na Kampuni ya KIRIBO.
Mgogoro ambao ulisababisha zuio la mgawo wa mawe hadi utatuzi ulipopatikana.

Waziri Mavunde ametumia takribani saa 6 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA).
“Ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini," amesema Mavunde.

Aidha, amezipongeza pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.
Ameongeza kwamba,kwa kuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu, ameelekeza zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho mapema tarehe 26.03.2024.

"Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya, wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao," amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.
Zaidi ya watu 2000 wananufaika na mgodi huo ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news