DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali itaendelea kudumisha utawala bora kwa kutumia sheria kama Msingi Mkuu wa Utendaji kazi wa serikali na haki za wananchi kwa ujuamla wake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea Jendwali la uchambuzi wa sheria ndogo kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Abdalla Dadi Chikota.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika kikao Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma
Waziri amesema hayo wakati akipokea Jendwali la uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Nne tarehe 2 Februari, 2024 tukio hilo limefanyika leo tarehe 22 Februari,2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge.