DODOMA-Baada ya ukaguzi wa matengenezo ya mitambo ya umeme Kidatu Mkoani Morogoro leo tarehe 1 Aprili, 2024 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembelea na kukagua Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Dkt.Biteko amewapongeza wataalamu kwa kazi kubwa ya kuendelea kufanya matengenezo ya haraka katika kituo cha kupoza Umeme cha Zuzu na maeneo yote yaliyokumbwa na kadhia hiyo kote nchini huku akisisitiza wataalamu kuendelea kukamilisha matengenezo kwa haraka ili umeme urejee maeneo yote ya nchi.