MAPUTO-Aprili 2,2024, Mhe. Phaustine Kasike ambaye ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alitembelewa na Mhe. Ndamage Donat, Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Msumbiji.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 3,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Mhe. Balozi Donate alifika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Maputo kujitambulisha kufuatia kuteuliwa hivi karibuni na nchi yake kuiwakilisha nchini Msumbiji.