ARUSHA-Mkutano Maalum wa 53 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika leo tarehe 25 Aprili 2024 Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
Mkutano huo, pamoja na masuala mengine umejadili na kupitisha Makadrio ya Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.).
Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb.) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.
Mkutano huo umefanyika kufuatia kukamilika kwa kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 24 Aprili 2024 ambacho kilitanguliwa na kikao cha ngazi ya Wataalam cha tarehe 23 Aprili 2024.