Bima ya Afya kwa Wote ni utekelezaji wa Sera ya Wazee-Dkt.Mollel

DODOMA-Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa kuanza kwa utekelezaji wa bima ya Afya kwa wote itakuwa suluhu ya kudumu ya utekelezaji wa Sera ya wazee kupata matibabu bure katika kila Kituo cha Afya nchini.
Dkt. Mollel amebainisha hayo kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15 na kikao cha kwanza wakati akijibu swali Namba 12 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maakum Mhe. Tauhida Cassian Gallos aliyeuliza Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika kila Kituo cha Afya nchini

“Wazee wasio na uwezo wa kugharamia huduma za Afya wameendelea kupatiwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha hata hivyo ni kweli kuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo,”ameeleza DKt. Mollel.

Dkt. Mollel ametoa wito kwa wabunge na madiwani kuhakikisha wanashirikiana ili kusimamia Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika maeneo yao ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa sera hiyo katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news