Bosi wa zamani Taifa Stars apewa ajira Super Eagles

ABUJA- Aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Emmanuel Amunike ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles).
Bosi wa zamani Taifa Stars. (Picha na The Citizen).

Julai 8,2019 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitangaza kusitisha mkataba na kocha huyo.

Aidha,taarifa fupi iliyotolewa na TFF wakati huo ilidai kuwa, Kocha Amunike alikubaliana na TFF kusitisha mkataba huo.

Kupitia ajira mpya, Kocha Amunike anakwenda kuchukua nafasi ya José Peseiro ambaye aling’oka kwenye kiti hicho baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON 2023 nchini Ivory Coast.

Kocha Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Taifa Stars mwezi Aprili, 2018 ambapo aliiongoza hadi kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya miaka 39.

Vile vile, kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria.

Kocha huyo ni winga wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Barcelona,Zamalek na Sporting Lisbon.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news