CFR NA IPA:Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar siku ya Aprili 24

DAR ES SALAAM-Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) na Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) kwa pamoja wanaandaa Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Ni kongamano lenye lengo la kuwaleta pamoja Viongozi na Wanazuoni kutoka pande zote mbili za Muungano.

Mada kuu katika Kongamano hilo ni "Miaka 60 ya Muungano katika Diplomasia na Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Buluu".

Kupitia mada hii washiriki watapata muda wa kujadili hali halisi ya Muungano katika Diplomasia na Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Buluu.

Aidha,kongamano hili limepangwa kufanyika tarehe 24 Aprili 2024 katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, uliopo Tunguu, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news