ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi yanayofanyika katika viwanja vya General Tyre vilivyopo Njiro jijini Arusha.
Maadhimisho hayo yameanza Aprili 23,2024 na yatamalizika Aprili 30,2024 yakiongozwa na kauli mbinu ya mwaka huu ya "Athari ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Usalama na Afya Kazini".
Pamoja na kutoa elimu ya dawa za kulevya kwa ujumla, maafisa wanazungumzia pia uhusiano mkubwa uliopo kati ya tatizo la dawa za kulevya na usalama na afya mahala pa kazi.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)