NA GODFREY NNKO
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imekamata zaidi ya kilo 767.2 za dawa za kulevya aina mbalimbali wakiwemo watuhumiwa 21.
Hayo yamesemwa leo Aprili 22,2024 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesema, dawa hizo zilikamtwa kwa nyakati tofauti kupitia operesheni iliyofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga kuanzia Aprili 4 hadi 18, mwaka huu.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema, kati ya dawa hizo zilizokamatwa Heroine ni kilogramu 233.2, Methamphemine kilogramu 525.67 na Skanka kilogramu 8.33.
"Watuhumiwa 21 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo za kulevya, baadhi yao wamefikishwa mahakamani na wengine watafikishwa taratibu za kisheria zitakapokamilika,"amefafanua Kamishna Jenerali Lyimo.
Amesema, watuhumiwa wanaowakamata wengi wapo katika kundi la vijana kuanzia miaka 20 hadi 35.
Tags
Breaking News
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)