Dkt.Tulia afungua kikao cha kujadili mabadiliko ya tabianchi jijini Washington DC

WASHINGTON DC-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua kikao cha kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba Dunia na utatuzi wake.Ni wakati wa Mkutano wa Mwaka 2024 wa Jukwaa la Kibunge la Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ulioanza tarehe 15 Aprili, 2024 katika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Washington DC, nchini Marekani.
Dkt. Tulia amesisitiza umuhimu wa Benki ya Dunia na IMF kuruhusu njia bora zaidi za kusaidia nchi zinazokumbwa na maafa ya mabadiliko ya tabianchi kupitia mfuko wa maafa.

Aidha, ameyaasa Mabunge kuwa chachu ya utekelezaji wa mkataba wa Mazingira wa Paris kwa vitendo zaidi kuliko majadiliano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news