DODOMA-Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza TEMESA itathmini mikakati mbadala ya kupunguza utegemezi wa vivuko vya mwendokasi kwakuwa kuendelea kukodisha vivuko hivyo kutoka Kampuni ya Azam Marine kunaathiri uendelevu wa huduma ambapo TEMESA inailipa Azam ada ya huduma kila siku Tsh. milioni 5 pamoja na kodi ya zuio ya 5%.
Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “Juni 14, 2022, Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania (TEMESA) uliingia mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya AZAM Marine Ltd ya kukodi na kuendesha vivuko viwili vya baharini 'Sea Taxi 1', na 'Sea Taxi 2' kati ya Magogoni na Kigamboni, mpango huu ulilenga kuongeza uwezo wa TEMESA kuhudumia Wateja kufuatia ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Magogoni”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo